Kinyanja
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinyanja (pia Chichewa) ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa nchini Malawi kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kinyanja nchini Malawi imehesabiwa kuwa watu milioni saba. Pia kuna wasemaji 803,000 nchini Zambia (2001), 599,000 nchini Msumbiji (2006), na 252,000 nchini Zimbabwe (1969). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyanja iko katika kundi la N30.