Hedmark
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hedmark ni moja kati ya majimbo ya Norwei. Jimbo hilo limepakana na Sør-Trøndelag, Oppland na Akershus.
Ngazi ya utawala ya jimbo hili ipo mjini Hamar.
Hedmark huwa upande wa kaskazini-mashariki mwa sehemu ya Østlandet, sehemu ya kusini ya jimbo. Inajumuisha sehemu ndefu ya mipaka ya Sweden, Jimbo la Dalarna na Jimbo la Värmland. Maziwa makubwa jimboni humo ni Femunden na Mjøsa. Pia inajumuisha sehemu za Glomma.
Kijiografia, Hedmark imegawanyika kizamani katika maeneo yafuatayo: Hedemarken, mashariki mwa Mjøsa, Østerdalen, kaskazini mwa Elverum, na Glåmdalen, kusini mwa Elverum. Hedmark na Oppland ni majimbo pekee nchini Norwei ambayo hayana ukanda wa pwani. Hedmark pia ishawahi kuandaa baadhi ya mashindano ya 1994 Winter Olympic Games.
Jimboni humo miji mashuhuri ni pamoja na Hamar, Kongsvinger, Elverum na Tynset. Hedmark ni moja kati maeneo ambayo hayakujengwa sana nchini Norwei, jinsi ilivyo nusu ya wakazi wake wanaishi katika maeneo ya vijijini. Uwingi wa watu hutazamwa sana kule katika maeneo ya matajiri ambapo ni Mjøsa na pande zingine za kusini-mashariki. Misitu mikubwa ya jimboni hapa inasambaza mbao vya kutosha nchini Norwei; vigogo vilikuwa vikisafirishwa kupitia Glomma kwa njia ya bahari lakini siku hizi vinasafirishwa kwa njia ya lori au treni.