Pennsylvania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pennsylvania ni jimbo la kujitawala la Muungano wa Madola ya Amerika au Marekani. Iko kaskazini-mashariki ya nchi ikipakana na majimbo ya Ohio, West Virginia, Maryland, Delaware, New Jersey na jimbo la New York. Kona ya kaskazini-magharibi yagusa Ziwa Erie na Kanada iko ng'ambo ya ziwa hili.
Pennsylvania Keystone State, Quaker State |
|||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Harrisburg | ||
Eneo | |||
- Jumla | 119,283 km² | ||
- Kavu | 116,074 km² | ||
- Maji | 3,208 km² | ||
Tovuti: http://www.pa.gov/ |
Mji mkuu ni Harrisburg lakini mji mkubwa ni Philadelphia. Kwa miji mingine, angalia Orodha ya miji ya Pennsylvania.
Jina la jimbo latokana na jina la William Penn aliyepewa ardhi ya kuanzisha makazi kwa ajili ya kundi la kidini la Maquaker. Jina la jimbo latafsiriwa kama "misitu ya Penn". Pennsylvania ilikuwa moja ya makoloni 13 asilia ya Uingereza yaliyoasi dhidi ya nchi mama baada ya mwaka 1776 na kuanzisha Muungano wa Madola ya Amerika .
Pennsylvania ina wakazi 12,281,054 kwenye eneo la 119,283 km². Zaidi ya nusu huishi katika maeneo ya miji mikubwa Pittsburgh na Philadelphia. Kaskazini ya jimbo ina watu wachache.
Sehemu kubwa ya eneo la jimbo ni milima ya Appalachi. Mito mikubwa ni Monongahela, Allegheny na Ohio.