Po (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Po ni mto mrefu zaidi nchini Italia, wenye urefu wa kilomita 652.
Ukweli wa haraka Mto Po ...
Mto Po | |
---|---|
| |
Chanzo | Milima ya Monviso |
Mdomo | Bahari ya Adria |
Nchi za beseni ya mto | Italia (100.0%) |
Urefu | 652 km |
Funga
Unapita kaskazini mwa Italia kuanzia chanzo chake katika milima ya Alpi kuelekea mashariki hadi mdomo wake kwenye bahari ya Adria karibu na mji wa Venisi.
Beseni lake huwa na eneo la km² 71,000.
Unapitia mikoa minne: Piemonte, Lombardia, Emilia-Romagna, Veneto. Hapo unapita kwenye miji muhimu kama vile Torino na karibu na Milano.
Mdomo wake huishia kama delta.