Raekwon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Corey Woods (amezaliwa 12 Januari, 1970) ni msanii wa rap na hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Raekwon (pia huitwa "Raekwon the Chef"). Huyu ni mmoja kati ya wanaounda kundi zima la muziki wa hip la Wu-Tang Clan. Alitoa albamu yake ya kwanza akiwa kama msanii wa kujitegemea mnamo mwaka wa 1995. Albamu ilikwenda kwa jina la Only Built 4 Cuban Linx..., na akaendelea kufanya shughuli zake akiwa kama msanii wa kujitegemea huku akiwa na washikaji zake wa Wu-Tang Clan. Mnamo mwaka wa 2009, Raekwon ametoa toleo la pili la albamu yake ya kwanza na kuipa sifa ileile, Only Built 4 Cuban Linx... Pt. II.
Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Raekwon The Chef | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Corey Woods |
Asili yake | New York City, New York, United States |
Aina ya muziki | Hip hop |
Miaka ya kazi | 1993 - mpaka sasa |
Studio | Loud, Universal, Aftermath, EMI Legion of D.O.O.M. |
Ame/Wameshirikiana na | Wu-Tang Clan |
Tovuti | www.myspace.com/raekwon |
Funga