Valencia CF
From Wikipedia, the free encyclopedia
Valencia Club de Fútbol (matamshi ya Kihispania: [balenθja kluβ ðe fuðβol], kwa kawaida hujulikana kama Valencia CF au Valencia tu) ni klabu ya soka ya Hispania iliyoko mjini Valencia.
Klabu hii ilianzishwa tarehe 5 Machi 1919 na kupitishwa tarehe 18 machi 1919 na Octavio Augusto Milego Díaz kama raisi wake wa kwanza.
Klabu ya Valencia inacheza katika La Liga.
Valencia imeongoza mara sita katika La Liga, mara saba katika Copa del Rey na mara mbili katika mashindano ya Inter-Cities Fairs Cups (mchezaji wa Kombe la UEFA). pia imechukua mara moja Kombe la UEFA.