Baba Sy
From Wikipedia, the free encyclopedia
Baba Sy (Donaye, Senegal, 1935 - Dakar, 20 Agosti 1978) alikuwa mchezaji wa bao wa Senegal na bingwa wa kwanza wa ulimwengu kutoka bara la Afrika.
Mnamo 1962, Ujerumani iliandaa mchezo mkubwa wa wachezaji bao. Sy alikuwa wa pekee kutoka Senegal, na Mwafrika Mweusi pekee. Alicheza dhidi ya mabingwa 150 kwa wakati mmoja, akikawia kwenye meza moja kwa sekunde chache tu kabla ya kwenda kwa nyingine.
Alifariki kwenye ajali ya barabarani kule Dakar. Alituzwa ubingwa wa ulimwengu akiwa ameshaaga dunia mnamo mwaka wa 1986.