Bata mchovya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mabata wachovya ni ndege wa majini wa nusufamilia Anatinae katika familia Anatidae.
Bata mchovya | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bata Domo-njano | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 17:
| ||||||||||||
Spishi hizi hula mimea ya majini na huzamia kichwa chao tu; nyingine hutafuta chakula aghalabu ardhini.
Miguu yao iko karibu zaidi ya katikati ya mwili kuliko miguu ya mabata wazamaji na kwa sababu hiyo wanaweza kutembea vizuri. Hutokea kwa makundi kwa maji baridi au milango ya mito.
Hujenga matago yao ardhini au ndani ya shimo. Wanaweza kuruka angani vizuri na spishi za kanda za kaskazini huhamia kusini kila majira ya baridi.
Uainisho wa Anatinae hauna hakika. Hapa jenasi kumi zimewekwa ndani ya familia ndogo hii zilizopo bado, na pia jenasi tatu zilizokwisha sasa. Visukuku vya spishi ndogo vimefunuliwa katika kisiwa cha Rota (Visiwa vya Mariana) ambayo inafanana na jenasi Anas.