Cherimiyo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Cherimiyo ni ndege wadogo wa jenasi Bias na Megabyas katika familia Platysteiridae wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara. Zamani waliainishwa katika familia Muscicapidae. Labda Bias ina mnasaba zaidi na milali (Prionopidae).
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Cherimiyo | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Cherimiyo rangi-mbili | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Funga
Kila jenasi ina spishi moja tu. Dume la spishi zote mbili ni mweusi juu na mweupe chini, lakini cherimiyo-mbwigu ana kishungi na koo lake ni jeusi. Jike ni kahawia au kahawiachekundu. Cherimiyo hula wadudu na hulijenga tago lao kwa majani, uvumwani na utando wa buibui na kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka. Jike huyataga mayai 2-4.