Jayne Atkinson
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jayne Atkinson (amezaliwa tar. 18 Februari 1959) ni mshindi wa Tuzo ya Tony, akiwa kama mwigizaji bora wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Karen Hayes kutoka katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24. Vilevile anafahamika kwa kucheza kama Theresa LePore katika filamu ya Recount. Kiasili, anatoka Uingereza, lakini wazazi wake walielekea Marekani akiwa na umri wa miaka tisa.
Ukweli wa haraka Amezaliwa, Miaka ya kazi ...
Jayne Atkinson | |
---|---|
Amezaliwa | 18 Februari 1959 (1959-02-18) (umri 65) Bournemouth, Uingereza |
Miaka ya kazi | 1987-hadi |
Ndoa | Michel Gill (1998-hadi leo) |
Tovuti rasmi |
Funga