Jiolojia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jiolojia (kutoka Kigiriki γῆ ge „ardhi“ na λόγος logos, somo, mafundisho“ = "geologia" - kwa matamshi ya Kiingereza "jiolojia") ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia. Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia.
Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 1778 na Mfaransa Jean-André Deluc (1727–1817).
Jiolojia inatazama mawe na ardhi ikitafuta maelezo kwa umbo na tabia zake kuligana na kanuni za kisayansi.
Kuna masomo madogo ndani ya jiolojia kama vile:
- Petrolojia ni elimu ya mawe na miamba
- Mineralojia ni elimu ya madini
- Jiolojia ya kihistoria ni elimu ya matokeo yaliyosababisha kutokea kwa mawe, miamba, milima na mabara jinsi yalivyo leo
- Paleontolojia ni elimu ya visukuku (mabaki ya miili ya wanyama wa kale yaliyokuwa kama mwamba)
- Hidrojiolojia ni elimu ya hali ya maji chini ya uso wa dunia
- Volkenolojia ni elimu ya volkeno kwenye mabara au chini ya bahari