Kasai
Kasai ni tawimto refu la Kongo unaoanza kwenye Nyanda za Juu za Bie za Angola. / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kasai ni tawimto refu la Kongo unaoanza kwenye Nyanda za Juu za Bie za Angola. Chanzo kiko kwenye 12° kus/19° kask. kaskazini ya mji wa Luena. Inaelekea magharibi km 400 inapogeukia kaskazini. Sasa iko mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Angola kwa 483 km. Katika sehemu hi kuna maporomoko makubwa kadhaa na lalio la mto unapanuka hadi 10 km.
Ukweli wa haraka Mto wa Kasai ...
Chanzo | Nyanda za juu za Bié (Angola) |
Mdomo | Kongo 170 km kaskazini ya Kinshasa |
Nchi | Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Urefu | 2,153 km |
Kimo cha chanzo | takriban 1,500 m |
Mkondo | hadi 12,000 m³/s |
Eneo la beseni | 881,890 km² |
Funga
Kabla ya kufikia Ilebo mto unageukia kuelekea magharibi-kaskazini. Sasa ni pia njia ya maji inayotumika na meli. Mto unapanuka kuwa bwawa la Wissmann. Karibu na mji wa Bandundu mto wa Kwango unajiunga na Kasai.
Sehemu ya mwisho mto umejulikana kwa jina la Kwa hadi kufika Kongo.