Maambukizi ya njia za mkojo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maambukizi ya njia za mkojo ni maambukizi ya bakteria katika njia za mkojo.
- Yanapoathiri sehemu ya chini ya njia hizo, maambukizi hayo hujulikana kama sisititisi ndogo (maambukizi ya kibofu).
- Yanapoathiri sehemu ya juu ya njia za mkojo, maambukizi hayo hujulikana kama pilonifritisi (maambukizi ya figo).
Maambukizi ya njia za mkojo | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Urology |
ICD-10 | N39.0 |
ICD-9 | 599.0 |
DiseasesDB | 13657 |
MedlinePlus | 000521 |
eMedicine | emerg/625 emerg/626 |
MeSH | D014552 |
Dalili katika sehemu ya chini ya njia za mkojo ni pamoja na uchungu wakati wa kukojoa na aidha kukojoa kila mara au kuhisi haja ya kukojoa (au zote mbili).
Dalili za maambukizi ya figo huhusisha pia homa na maumivu ya fumbatio (mwanya wa fupanyonga). Katika wazee na watoto wachanga, dalili haziwi wazi kila wakati.
Kisababishi kikuu cha aina hizo mbili niEscherichia coli. Hata hivyo, katika matukio machache, bakteria wengineo, virusi au kuvu wanaweza kuwa ndivyo visababishi.
Maambukizi ya njia za mkojo huwatokea mara nyingi zaidi wanawake kuliko wanaume. Nusu ya idadi ya wanawake huambukizwa wakati fulani maishani mwao. Marudio hutokea mara nyingi. Vipengele visababishi vilivyo hatari ni pamoja na ngono na pia historia ya kifamilia. Maambukizi ya figo yanaweza kufuatia maambukizi ya kibofu, pia yanaweza kusababishwa na maambukizi ya damu.
Utambuzi katika wanawake wachanga wenye afya unaweza kutazamwa kwa msingi wa dalili pekee. Utambuzi unaweza kuwa mgumu kwa watu walio na dalili zisizo wazi kwani bakteria wanaweza kuwepo hata kama mtu huyu hana maambukizi. Katika matukio yenye matatizo au ikiwa matibabu hayajafaulu, uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati mwingine husaidia. Mtu aliye na maambukizi ya kila mara anaweza kutumia kipimo kidogo cha antibiotiki kama namna ya kuzuia.
Matukio madogo ya maambukizi katika njia za mkojo hutibiwa kwa urahisi kwa kutumia mfululizo wa antibiotiki. Hata hivyo usugu dhidi ya antibiotiki zinazotumika kutibu hali hii, unaendelea kuongezeka. Watu walio na matukio yenye matatizo, wakati mwingine hushurutika kutumia antibiotiki kwa muda mrefu zaidi au watumie antibiotiki zinazodungwa ndani ya misuli. Ikiwa dalili hazipungui baada ya siku mbili au tatu, mtu atahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi. Katika wanawake, maambukizi ya njia za mkojo ndiyo maambukizi yanayotokea mara nyingi zaidi katika aina zote za maambukizi ya bakteria. Asilimia kumi ya wanawake hupata maambukizi ya nia za mkojo kila mwaka.