Yosia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosia (kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake "aliyeponywa na YHWH" au "aliyetegemezwa na Yah"[1][2]; kwa Kigiriki: Ιωσιας; kwa Kilatini: Josias; 649 KK – 609 KK) alikuwa mfalme wa 16 wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika wakati huo, kwa mchango wake pia.
Hasa alitumia nguvu zake zote kutekeleza agizo la gombo lililopatikana mwaka 622 KK likidai sadaka zote zitolewe katika hekalu la Yerusalemu tu, kadiri ya msimamo wa Kumbukumbu la Torati: "Mungu mmoja, hekalu moja".
Ndiyo maana Biblia inamsifu kwa namna ya pekee pamoja na Hezekia kati ya wafalme wote wa Israeli na Yuda, mbali na Daudi aliyebaki kielelezo cha kudumu cha mtawala aliyempendeza Mungu.