Michoacán
From Wikipedia, the free encyclopedia
Michoacán ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko. Mji mkuu na mji mkubwa ni Morelia.
Imepakana na Colima, Jalisco, Guanajuato, Querétaro, Mexico na Guerrero. Upande wa kusini kuna pwani na Pasifiki. Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 3,966,073. Una eneo la 59,864km².
Michoacán ni jimbo yenye historia udefu. Wap'urhépecha ilikuwa jina la ustaarabu muhimu wa kienyeji katika eneo la jimbo kabla ya kufika kwa Wahispania.
Gavana wa jimbo ni Salvador Lopez Orduna.
Lugha rasmi ni Kihispania.