Mkoa wa Pwani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 61000.
Kwa mkoa wa zamani wa Kenya, tazama Mkoa wa Pwani (Kenya).
Mkoa umepakana upande wa Kaskazini na Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro.
Makao makuu ya mkoa yako Kibaha.