Nabii Hagai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nabii Hagai (kwa Kiebrania חַגַּי, Ḥaggay au "Hag-i", yaani Sikukuu yangu; kwa Kigiriki: Ἀγγαῖος; kwa Kilatini Aggeus) ni mmojawapo kati ya manabii wa Israeli, aliyetoa ujumbe wake miezi ya mwisho ya mwaka 520 KK tu, akihimiza pamoja na nabii Zekaria ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu baada ya Wayahudi kurudi toka uhamisho wa Babeli.
Hatimaye kazi hiyo ilikamilika na hekalu likatabarukiwa mwaka 515 KK.