Nuevo León
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nuevo León (León mpya, ufalme wa kale katika Hispania) ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kaskazini-mashariki ya nchi. Mji mkuu na mji mkubwa ni Monterrey.
Imepakana na Coahuila, Tamaulipas na San Luis Potosí. Upande wa kaskazini kuna mpeka na Marekani (kilomita 15 pekee).
Jimbo lina wakazi wapatao 4,199,292 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 64,210.
Gavana wa jimbo ni Natividad González Parás.
Lugha rasmi ni Kihispania.