Shelly-Ann Fraser
From Wikipedia, the free encyclopedia
Shelly-Ann Fraser, OD (alizaliwa 27 Desemba 1986) ni mwanariadha wa nchi ya Jamaika ambaye amebobea katika mbio ya 100m. Alizaliwa katika jiji la Kingston, Jamaika, Fraser ndiye bingwa mtetezi wa Olimpiki na Dunia katika mbio ya 100m, akikimbia katika muda wa 10.78s (Olimpiki) na 10.73s (Dunia). Yeye ndiye mwanamke pekee aliyeshikilia mataji ya ubingwa wa Olimpiki na Dunia yote mawili kwa wakati mmoja. Ametoshana na Christine Arron kama mwanamke wa nne wa kasi kabisa katika historia ya mbio ya 100m. Alisoma katika Shule ya Upili ya Wolmer's ya Wasichana na akawakilisha shule yake katika mashindano mengi ya riadha.
Ukweli wa haraka Rekodi za medali, Anawakilisha nchi Jamaika ...
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Anawakilisha nchi Jamaika | ||
Riadha ya Wanawake | ||
Michezo ya Olimpiki | ||
Dhahabu | 2008 Beijing | Mbio ya mita 100 |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF | ||
Dhahabu | 2009 Berlin | Mbio ya 100 m |
Dhahabu | 2009 Berlin | Mbio ya 4 x 100m |
Fedha | 2007 Osaka | Mbio ya 4 x 100m |
Funga