Sierra Nevada, Hispania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuhusu milima nchini Marekani angalia hapa Sierra Nevada
Sierra Nevada (Kihispania kwa "milima ya theluji") ni safu ya milima katika mkoa wa Andalusia nchini Hispania. Mlima wake mkubwa ni pia mlima mkubwa kabisa wa Hispania ambao ni Mulhacén wenye kimo cha mita 3,479 juu ya u.b.
Ni kivutio maarufu cha watalii. Milima mirefu inawezesha kucheza skii hivyo kuna utalii wa skii wa kusini zaidi kwenye bara la Ulaya ukiwa karibu na bahari ya Mediteranea.
Miguuni pa milima kuna miji ya Granada na, kwa umbali kidogo, Málaga na Almeria.