Ufini
nchi katika Ulaya Kaskazini / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ufini (kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: none | |||||
Wimbo wa taifa: Maamme (Kifini) Vårt land (Kiswidi) ("Nchi yetu" Kiswahili) | |||||
Mji mkuu | Helsinki 60°10′ N 24°56′ E | ||||
Mji mkubwa nchini | Helsinki | ||||
Lugha rasmi | Kifini (89.33%), Kiswidi (5.34%) | ||||
Serikali | Jamhuri2 Alexander Stubb Petteri Orpo | ||||
Uhuru imetangazwa |
6 Desemba 1917 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
338,145 km² (ya 64) 9.4 | ||||
Idadi ya watu - 2014 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
5,470,820 (ya 115) 5,181,115 16/km² (ya 201) | ||||
Fedha | Euro (€)1 (EUR ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | [.fi] | ||||
Kodi ya simu | +358
- | ||||
1Prior to 1999: Finnish markka 2Semi-presidential system |
Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.
Ufini ilijitegemea mnamo 1917. Kati ya 1939 na 1944, Ufini ilipigana dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na jeshi la Ufini liliongozwa na kamanda Carl Gustaf Emil Mannerheim.
Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.