Ulaanbaatar
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ulaanbaatar (pia: Ulan Bator; Kimongolia Улаанбаатар - "mshujaa mwekundu") ni mji mkuu wa Mongolia mwenye wakazi 844,818. Sehemu ya wakazi hufuata mapokeo ya Mongolia wakiishi mjini miezi ya baridi tu lakini miezi ya joto huhamahama kwenye hema pamoja na mifugo yao.