Wakartusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Shirika la Wakartusi, au Shirika la Mt. Bruno, ni utawa mmojawapo wa Kanisa Katoliki. Wamonaki wake wote, wanaume kwa wanawake wanaishi ndani kwa ndani: wengine katika nyumba za binafsi, wengine katika makao ya pamoja.
Shirika lilianzishwa na Bruno Mkartusi mwaka 1084.
Linafuata sheria zake, badala ya kanuni ya Benedikto wa Nursia inayoongoza wamonaki karibu wote wa Kanisa la Kilatini.
Jina linatokana na milima ya Chartreuse (nchini Ufaransa), ambapo Bruno na wakaapweke wenzake 6 walijenga makao ya kwanza.
Kaulimbiu ya shirika ni: Stat crux dum volvitur orbis (kwa Kilatini "Msalaba unadumu wakati ulimwengu unabadilikabadilika."