Agnes Cao Guiying
From Wikipedia, the free encyclopedia
Agnes Cao Guiying (Wujiazhai, 1821 hivi - Xilin 1 Machi 1856) alikuwa mwanamke mjane wa China aliyefia Ukristo.
Baada ya kufiwa mume wake mkorofi, alitumwa na askofu kufundisha katekesi ya Kikristo. Kwa sababu hiyo alifungwa gerezani alipovumilia mateso ya kikatili sana akimtegemea daima Mungu.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, ila ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[1].