Basmala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Basmala (Ar. بسملة basmala) ni jina kwa maneno ya Bismillah (بسم الله "Kwa jina la Mungu/Allah", kamili "b-ismi-llāhi r-raḥmāni r-raḥīmi") ambayo ni maneno ya ufunguzi kwa sura za Qurani[1]. Ar-rahman („mwenye rehema“) na Ar-rahim („mwenye neema“) ni pia kati ya majina 99 ya Allah.
Waislamu hutumia maneno haya mara nyingi kwa mfano kila wanapoanza sala au kazi muhimu kama vile kabla ya kula chakula, kabla ya safari, wakati wa kuingia katika msikiti, wakati wa kuzika maiti.
Katika sanaa ya Kiislamu basmala hutumiwa mara nyingi kama kaligrafia.