Fransisko Serrano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Serrano, O.P. (Hueneja, 4 Desemba 1695 – Fuzhou, 25 Oktoba 1748) alikuwa askofu kutoka Hispania aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo.[1]
Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Oktoba, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai[3].