Ghostface Killah
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dennis Coles (amezaliwa tar. 9 Mei 1970)[1] ni msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ghostface Killah. Huyu ni mmoja kati ya wanaounda kundi zima la Wu-Tang Clan. Baada ya kundi kuambulia mafanikio yake makubwa kwa kutoa albamu yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Enter the Wu-Tang (36 Chambers) , huyu bwana naye akaamua kujiendeleza mwenyewe akiwa kama msanii wa kujitegemea na kuweza kupata mafanikio kibao. Ghostface Killah akatoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ironman, ambayo ilipokewa vyema sana na watathmini wa masuala ya muziki. Akaendeleza kazi yake, na kutengeneza albamu zake zilizojishindia tuzo kemekem. Albamu hizo ni pamoja na Supreme Clientele, Fishscale, na The Big Doe Rehab.
Ghostface Killah | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Dennis Coles |
Pia anajulikana kama | Tony Starks, Ironman, General Tony Starks, Pretty Toney, The Wallabee Kingpin, GFK, Ghost Deini, Starky Love, P Tone, Sun God, Wally Champ |
Amezaliwa | 9 Mei 1970 (1970-05-09) (umri 54) |
Asili yake | Staten Island, New York, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Miaka ya kazi | 1991–mpaka sasa |
Studio | Razor Sharp, Epic, Starks Enterprises, Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | Wu-Tang Clan, Theodore Unit, MF DOOM, Rakim, Adult Swim |
Tovuti | Ghostface's official site |
Ghostface Killah ni maarufu mno[2][3] kwa staili yake ya sauti kubwa, kuchana kwa haraka-haraka, na staili yake ya kuimba kama hataki huku akiwa anatia mbwembwe za maneno ya kitaa-kistori fulani ya kujitambua.[4][5]