Laurenti Bai Xiaoman
From Wikipedia, the free encyclopedia
Laurenti Bai Xiaoman (Guiyang, 1802 hivi - Maokou 25 Februari 1858) alikuwa fundi wa China aliyefia Ukristo, dini yake mpya, kwa kukatwa kichwa.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 25 Februari[1].