Lusia Wang Cheng
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lusia Wang Cheng (Laochuntan, 1882 hivi - Wangla 28 Juni 1900) alikuwa bikira wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Mabondia pamoja na Maria Fan Kun, Maria Qi Yu na Maria Zheng Xu. Kisha kulelewa katika kituo cha mayatima, walichomwa kwa upanga huku wakishikana mikono kuelekea kifodini na wakifurahi kama kwa kwenda kuolewa[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].