Malaika Mikaeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Malaika Mikaeli (kwa Kiebrania מִיכָאֵל, Micha'el au Mîkhā'ēl, maana yake Nani kama Mungu; kwa Kigiriki Μιχαήλ, Mikhaḗl; kwa Kiarabu ميخائيل, Mīkhā'īl) anaheshimiwa kama malaika mkuu katika imani ya dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
Katika Biblia ya Kiebrania anatajwa mara tatu katika Kitabu cha Danieli.
Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo anatajwa katika Waraka wa Yuda na katika Kitabu cha Ufunuo.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Septemba[1][2]