Mchungaji mwema
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mchungaji mwema (kwa Kigiriki: ποιμήν ο καλός, poimḗn o kalós) ni namna mojawapo ya Yesu kuwaeleza wafuasi wake yeye ni nani kwao. Ufafanuzi wake unapatikana katika Yoh 10:1-21, anapojitofautisha na wachungaji (yaani viongozi) wabaya, kwa kusema yeye yuko tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo (watu) wake[2].
Maelezo zaidi Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu, Mazingira ya Yesu ...
Funga
Lugha hiyo inategemea Zaburi 23 na sehemu nyingine ya Agano la Kale. Pia inatumika katika Injili nyingine, Waraka kwa Waebrania, Waraka wa kwanza wa Petro na kitabu cha Ufunuo][3].
Mfano huo uligusa sana Wakristo na kuchochea usanii wao tangu mwanzo.