Morisi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Morisi ni kisiwa karibu na Afrika, pia ni nchi inayoitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (kwa Kiingereza: Republic of Mauritius, kwa Kifaransa: République de Maurice). Ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban Km 900 mashariki kwa Madagaska na km 4000 kusini-magharibi kwa Bara Hindi.
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Stella Clavisque Maris Indici (Kilatini: Nyota na ufunguo wa Bahari Hindi) | |||||
Wimbo wa taifa: Taifa | |||||
Mji mkuu | Port Louis 20°10′ S 57°31′ E | ||||
Mji mkubwa nchini | Port Louis | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kifaransa | ||||
Serikali Rais Waziri Mkuu |
Jamhuri Prithvirajsing Roopun Pravind Jugnauth | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
12.03.1968 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,040 km² (ya 169) 0.05 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
1,265,475 (ya 156) 1,259,838 618/km² (ya 19) | ||||
Fedha | Mauritian Rupee (MUR ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .mu | ||||
Kodi ya simu | +230
- |
Funga
Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.
Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega.
Hivyo vyote ni sehemu ya funguvisiwa la Maskarena pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.
Mji mkuu wa jamhuri ni Port Louis.