Paulo Liu Hanzuo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Paulo Liu Hanzuo alikuwa padri wa China aliyefia Ukristo kwa kunyongwa huko Chengdu 13 Februari 1818.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu mfiadini mwaka 2000.
Sikukuu yake na ya wenzake 119 huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[1].