Pere Sans Jorda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pere Sans Jorda, O.P. (Asco, 3 Septemba 1680 – Fuzhou, 26 Mei 1747) alikuwa askofu kutoka Hispania aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo.[1]
Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai[3].