Petro Wu Guosheng
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro Wu Guosheng (Longping, 1768 hivi - Longping 7 Novemba 1814) alikuwa mlei katekista wa China aliyefia Ukristo kwa kunyongwa.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, ila ya kwake mwenyewe tarehe 7 Novemba[1].