Saba abati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Saba Abati (Mutalaska, karibu na Caesarea Mazaca, Kapadokia, leo nchini Uturuki, 439 – Yerusalemu, leo nchini Israeli/Palestina, 532), alikuwa mmonaki padri aliyeanzisha monasteri kadhaa, ambazo kati yake maarufu zaidi ni ile yenye jina lake (Mar Saba).[1]
Tangu kifo chake anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.