Sesilia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sesilia (kwa Kilatini Caecilia) alikuwa mwanamke Mkristo wa mjini Roma katika karne ya 2 na ya 3 BK.
Anaheshimiwa kama mtakatifu bikira mfiadini na somo wa wanamuziki kwa sababu inasimuliwa kwamba hao walipokuwa wakiimba kwenye arusi yake, mwenyewe "alikuwa akimuimbia Bwana moyoni".[1][2][3]
Sikukuu yake inaadhimishwa na madhehebu mbalimbali tarehe 22 Novemba.[4][5][6]