Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia hapa Tandala (Makete)
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Tandala |
Dume la tandala mkubwa (Tragelaphus strepsiceros) |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
|
Nusuoda: |
Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
|
Familia: |
Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe) J. E. Gray, 1821 |
Jenasi: |
Tragelaphus (Nyala, pongo na tandala) de Blainville, 1816 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 8:
- T. angasii Angas, 1849
- T. buxtoni (Lydekker, 1910)
- T. eurycerus (Ogilby, 1837)
- T. e. eurycerus (Ogilby, 1837)
- T. e. isaaci (Thomas, 1902)
- T. imberbis (Blyth, 1869)
- T. scriptus (Pallas, 1766)
- T. spekii (Speke, 1863)
- T. s. gratus (Sclater, 1880)
- T. s. selousi (Rothschild, 1898)
- T. s. spekii (Speke, 1863)
- T. strepsiceros (Pallas, 1766)
- T. s. chora (Cretzschmar, 1826)
- T. s. cottoni (Dollman & Burlace, 1928)
- T. s. strepsiceros (Pallas, 1766)
- T. sylvaticus (Sparrman, 1780)
|
Funga
Tandala (kwa Kiingereza: kudu) ni wanyama wa jenasi Tragelaphus katika familia Bovidae. Spishi nyingine huitwa bongo, kulungu, malu, nyala au nzohe.
Wanatokea Afrika katika maeneo yenye miti kutoka nyika hadi msitu.
Wana milia na madoa meupe juu ya rangi ya kahawa au kijivu. Dume ni mkubwa kuliko jike na ana pembe ndefu zilizopotolewa. Jike hana pembe.
Wanyama hao hula majani, manyasi, matunda na viazi vya gugu.