Yohane Alcober
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Alcober, O.P. (Granada, 21 Desemba 1694 – Fuzhou, 28 Oktoba 1748) alikuwa padri kutoka Hispania aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo.[1]
Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai.