Yohane Petro Neel
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Petro Neel, M.E.P. (Soleymieux, 18 Oktoba 1832 – Kaiyang, 18 Februari 1862) alikuwa padri kutoka Ufaransa aliyefanya umisionari barani Asia akauawa kwa kuburuzwa kwanza na farasi mwenye kasi na hatimaye kukatwa kichwa kwa sababu ya kuhubiri nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo.[1]
Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai[3].