Yosefu Zhang Dapeng
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Zhang Dapeng (Duyun, 1754 hivi - Guiyang 12 Machi 1815) alikuwa mlei katekista wa China aliyefia Ukristo kwa kusulubiwa.
Alipopokea mwanga wa imani, mara baada ya kubatizwa aliwafungulia nyumba yake wamisionari na makatekista akasaidia kwa kila namna watu fukara, wagonjwa na watoto. Alipopelekwa kwenye mateso ya msalabani, alimwaga machozi ya furaha kwa kujaliwa neema ya kumfia Yesu.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 12 Machi[1].