Yosefu wa Anchieta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu wa Anchieta (kwa Kihispania: José de Anchieta y Díaz de Clavijo, S.J.; San Cristóbal de La Laguna, Tenerife, Visiwa vya Kanari, Hispania, 19 Machi 1534 – Reritiba, Brazil, 9 Juni 1597) tangu ujanani alikuwa mmisionari katika koloni la Brazil katika karne ya 16[1].
Pamoja na mwenzake Manuel da Nóbrega alisaidia Waindio wengi kuingia Ukristo[2] na kuwapatanisha na wakoloni Wareno.
Anchieta ni kati ya waanzilishi wa jiji la São Paulo (1554) na Rio de Janeiro (1565) lakini pia wa fasihi ya Kibrazil[3].
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 22 Juni 1980, halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 3 Aprili 2014[4][5].