Albinus wa Angers
From Wikipedia, the free encyclopedia
Albinus wa Angers (kwa Kifaransa: Aubin; Vannes, leo nchini Ufaransa, 496 hivi - Angers, 1 Machi 550) alikuwa kwanza mmonaki, halafu abati kwa miaka 25 na hatimaye askofu wa mji huo kuanzia mwaka 529[1], akijitahidi kurekebisha Kanisa kufuatana na mtaguso wa tatu wa Orleans na kutetea fukara na wafungwa hata kwa kukemea vikali fahari ya matajiri[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[3].