Anatolia na Viktoria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Anatolia na Viktoria (walifariki katika eneo la Lazio ya leo, Italia, 250 hivi) walikuwa wasichana Wakristo waliouawa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1][2].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.