Antifona
From Wikipedia, the free encyclopedia
Antifona (kwa Kiingereza "antiphon", kutoka Kigiriki ἀντίφωνον, ambamo mna: ἀντί "kinyume" na φωνή "sauti") ni aya inayotumika mwanzoni, lakini pia mwishoni na pengine hata mara kadhaa katikati ya Zaburi au wimbo mwingine katika ibada za Ukristo.
Mara nyingi antifona inakaririwa na kwaya au mkusanyiko wote wakati beti zinaimbwa na mwimbaji pekee[1].