Dini nchini Eritrea
From Wikipedia, the free encyclopedia
Dini nchini Eritrea hasa ni Dini za Abrahamu. Tangu Mei 2002, serikali ya Eritrea imetambua rasmi Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea (Tewahedo), Kanisa Katoliki la Eritrea, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri na Uislamu tu.
Maelezo zaidi U.S Department of State 2011, Pew Research 2009 ...
Funga
Imani na madhehebu mengine yote yanatakiwa kufuata mchakato wa usajili; lakini yale ambayo yanajulikana kama ni madhehebu ya kawaida na yapo duniani, basi hayana haja ya kujisajili.[3]
Miongoni mwa mambo mengine ni pamoja na muundo wa serikali kutaka kuwasilisha nyaraka binafsi za wanachama wa kikundi cha dini ili waruhusiwe kuabudu.