Esuperansi wa Ravenna
From Wikipedia, the free encyclopedia
Esuperansi wa Ravenna (430 hivi - Ravenna, Emilia-Romagna, Italia, 29 Mei 477) alikuwa askofu wa 19 wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 458 hivi, wakati Italia nzima ilipotekwa na Waostrogoti[1].
Katika mazingira hayo magumu aliongoza Kanisa kwa busara kubwa.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.