Eusebi wa Milano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Eusebi wa Milano (alifariki Milano, Italia Kaskazini, 8 Agosti 462) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 449.
Inasemekana alikuwa Mgiriki.
Alipigania imani sahihi na kujenga upya kanisa kuu lililobomolewa na Wahunni[1].
Papa Leo I alimuandikia barua (451).
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.