Fungo-bukini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fungo-bukini ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa Madagaska wanaoainishwa katika nusufamilia Euplerinae wa familia Eupleridae na ambao wanafanana na fungo wa bara la Afrika. Pamoja na nguchiro-bukini (nusufamilia Galidiinae) wana mhenga mmoja aliyekuwa aina ya nguchiro na aliyevuka Mlango wa Msumbiji miaka milioni 20 iliyopita.
Fungo-bukini | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fosa (Cryptoprocta ferox) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 3, spishi 4:
| ||||||||||||||
Wanyama hawa ni kama fungo wadogo au nguchiro, isipokuwa fosa. Mdogo kuliko wote ni fungo-bukini miraba (sm 20 na g 1500-2000) na mkubwa ni fosa (sm 70-80 na kg 5.5-8.6). Rangi yao ni kahawia au kahawianyekundu.
Wanatokea misituni na hula vertebrata kama lemuri, tandaraka, wagugunaji, mijusi na ndege (fosa na fungo-bukini miraba) au invertebrata kama nyungunyungu, konokono, konokono uchi na lava (falanuki).