Gildadi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gildadi (kwa Kifaransa: Gildard, Godard; Salency, 448 hivi – Rouen, Ufaransa, 525 hivi) alikuwa askofu wa 14 wa Rouen[1][2], wa kwanza kutoka kabila la Wafaranki waliovamia Galia[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4][5].